Fainali ya FA 2019

LEO itashuhudiwa fainali ya kombe linalofahamika kwa kuwa na uwekezaji wa aina yake ndani ya taifa la Uingereza ambapo mabingwa wa kombe la ligi, Manchester City wataumana vikali na Watford ambao hawajapata taji lolote msimu huu hivyo hiyo ni nafasi ya pekee kwao kuweza uonesha uwezo wao uwanjani.

Ndani ya mechi hiyo City wanaingia kwa kujiamini sana wakiwa na kikosi ambacho kwa hakika tunaweza kukiita ni cha kimashindano kutokana na uwezo wao wa kutetea ubingwa wa ligi ambao wameutwaa karibuni ndani ya taifa hilo la Uingereza wakiweza kuwapiku Liverpool.

Kubwa kutokea

Mbali na tukio hilo pia kuna jambo kubwa na la kihistoria litatokea ndani ya mechi hiyo ambapo mlinzi kisiki na mkongwe wa klabu hiyo, Vicent Kompany anaangaliwa kuagana na mashabiki zake wa muda mrefu mara baada ya kuwatumikia klabuni hapo kwa kipindi kirefu na kwa mafanikio makubwa.

Watu wanaokumbukwa kwa kuifanya klabu hiyo iweze kushinda taji hilo ni Carlos Tevez na Yaya Toure ambao kwa hakika waliweza kufanya vizuri zaidi na klabu hiyo ambayo hadi leo wanawaenzi kwa namna ya pekee wachezaji hao ndani ya kikosi chao hicho. Na hata waliyoyafanya bado yanabaki historia kubwa sana kwao.

Wamepata nafasi hiyo baada ya kuiongoza klabu hiyo kuchukua ushindi mbele ya Manchester United kwenye hatua ya nusu fainali na kusonga mbele hadi hatua ya fainali ambapo watakuwa Wembley leo kumenyana na Watford huku pia akiweza kuwaaga kwa huzuni mashabiki wake.

City watapigana kwa namna yoyote ili kiongozi wao huyo wa muda wote aweze kuondoka vizuri klabuni hapo huku akiwa amenyanyua kombe la pili ndani ya mwezi mmoja. Jambo hilo litaweza kumuacha salama zaidi Kompany hata ile ahadi ambayo wamewekeana na Pep ya kuagana vizuri na nyota huyo baada ya ushindi itatimia vizuri.

Utabiri ukoje?

Mechi hiyo ya leo inawapa asilimia nyingi Manchester City kutokana na uwezo wao mkubwa katika msimu huu, pia, jambo jingine wana kila sababu ya kulinyanyua kutokana na aina ya mpinzani wanayekutana naye kwenye nafasi yao hiyo.

Kwa namna moja au nyingine tunaweza kusema matokeo ya mechi hiyo hayatakuwa na cha kushangaza.

2 Komentara

    Man city lazima achukue.

    Jibu

    City kombe lao hlo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.