Timu ya taifa ya Hispania imeweka wazi kikosi chake kitakachoumana uwanjani kwenye michuano inayowakabili hapo mbeleni, ndani ya kikosi chao kuna maingizo mapya kabisa ya baadhi ya nyota ambao awali walikuwa hawajapata nafasi ndani ya kikosi hicho lakini kwa sasa wameaminiwa kupewa hiyo nafasi.
Ndani ya kikosi hicho pia ameonekana nyota wa zamani wa Arsenal ambaye kwa hakika ameweza kufanya kazi kubwa ndani ya msimu huu akiwa na klabu yake ya Villareal anayoitumikia baada ya kuachana na Arsenal kwa miaka mingi iliyopita. Ameamiiniwa na kujumuishwa na kikosi hicho.
La Roja watakuwa na mechi mbili watakazozicheza mapema Juni, 7 ambapo watasafiri hadi Faroe Islands ambako watacheza mechi yao watarejea na siku tatu baadaye watakabiliana na Sweden ambapo kwa hakika sio timu ya kubeza na wanaweza kuwaletea madhara makubwa kutokana na uzuri wa kikosi chao.
Katika majina hayo nyota Santi Cazorla amejumuishwa ndani ya kikosi hicho akiwa ni sehemu ya wachezaji watakaokabidhiwa timu na kuhakikisha inafanya vizuri kwa kuutawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho na kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mechi zao hizo.
Ni mara ya kwanza kwa nyota huyo kuitwa katika majukumu hayo ya kimataifa ikiwa ni tangu mwaka 2015 alipokuwa kama mchezaji wa Arsenal lakini kwa siku za hivi karibuni ameonesha kiwango cha juu sana na kumshawishi mwalimu hadi akafikia uamuzi wa kumuita kikosini.
Carzola (34) ndani ya ligi amefunga magoli manne na kuchangia upatikanaji wa magoli 10 katika mechi zake 34 alizoingia uwanjani. Mbali na hilo atakumbukwa sana na mashabiki wa Barcelona kutokana na makubwa aliyoyafanya wakati wa mechi yao hadi kupelekea kutoa sare ya 4-4.
Mbali na nyota huyo, wengine waliopewa nafasi kukijenga kikosi hicho ni: safu ya walinda mlango ina majina ya watu kama De Gea, Kepa, na Lopez ambao watakuwa na jukumu zito kuhakikisha wanaweka usalama wa kutosha kwenye lango ili kuzuia timu yao kusonga mbele.
Safu ya ulinzi ina watu kama: Ramos, Hermoso, Llorente, Carvajal, Alba, Navas, Martinez, Gaya, na Roberto; huku viungo kukiwa na Cazorla, Busquets, Parejo, Fabian, Isco, Oryazabal, na Rodri; na safu ya ushambuliaji ikikamilishwa na Rodrigo, Aspas, Morata, na Asensio wote hawa wakiwa ni vijana wenye umri wa chini kabisa.


Povel
Kikosi kipo poa sana