Fei Toto Atakiwa na TP Mazembe

Dili la kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo, la kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ limenoga zaidi huko Yanga, ambapo taarifa zimeeleza kuwa tayari viongozi wa klabu hiyo wameshawasilisha dau na kumnasa kwenye dirisha la usajili lijalo.

Mazembe wamezidi kuvutiwa na uwezo wa Fei Toto kiasi kwamba sasa wanasuburia tamko la Yanga tu ili waweze kumwaga pesa.

Chanzo kimeeleza kuwa hatimaye sasa Mazembe wameamua kuleta ofa maalumu kwa uongozi wa Yanga kuhusu kumsajili Fei.

“Ama kweli kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho, kwani pamoja na kuwepo na tetesi nyingi kiasi cha baadhi ya watu kubeza juu ya dili hilo, nikueleze tu kwamba mechi ya Stars imeongeza chachu ya TP Mazembe kumtaka Fei Toto.

“Kwani kilichobaki sasa ni kwetu viongozi kukubaliana juu ya ofa yao ili nasi tuweze kufaidi matunda ya kuuzwa kwake, TP Mazembe wametoa dau la Sh milioni 200 ili wavunje mkataba wake, ila sisi tunadhani wanatakiwa kuongeza hadi ifike Sh milioni 300 na kitu hivi ili tuwapatie jembe letu,” kilisema chanzo hicho.

Feti Toto alionyesha uwezo wa juu kiasi cha kuwavutia wengi katika mchezo wa Novemba 17 dhidi ya Tunisia, ambapo alifunga bapo la kusawazisha la Stars mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

28 Komentara

    Kila la kheri kama Tp mazembe watafanikiwah kupata sain Feisal TOTO

    Jibu

    Hlo ni shavu

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Fursa hyo Fei toto itumie

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Fursa nzuri sana kwa fei

    Jibu

    Fei toto ni jembe hatari kiukweli anauwezo mkubwa sana.

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Good

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Itakuwa Ni jambo zur san kwake

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Uwamuzi ni wake na uongozi wake kila la heri kwake

    Jibu

    Safi sana Feisal kambi popote kaka

    Jibu

    Safi

    Jibu

    safi sana kijana nenda kaongeze kiwango kikubwa zaidi uko

    Jibu

    Safii Sana dogo nenda kapige kazi ndio mwanzo wakutoka huo maisha kutafuta

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Shavu hilo kwa Fei toto

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Kila la kher

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Kiungo hakuna anaefanana nae afrika masharik

    Jibu

    Kaza buti kijana

    Jibu

    Fei anajitahid sana

    Jibu

Acha ujumbe