Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa hawezi kubadilisha matokeo aliyoyapata kwa timu yake kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Simba kwa kuwa yameshatokea kutokana na makosa ya kujirudia kwa wachezaji wake ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Coastal Union inaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwa msimu wa 2020/21 kufungwa mabao mengi bila safu yake ya ushambuliaji kuambulia bao kwa kuwa timu ya kwanza iliyofungwa mabao mengi ilikuwa ni Mwadui FC iliyofungwa mabao 6-1 na JKT Tanzania.

Mabao kwa upande wa Simba yalifungwa na Hassan Dilunga ambaye bao lake lilileta utata kutoka kwa wachezaji wa Coastal Union ambao walionekana kumfuata mwamuzi wa kati wakidai kwamba mfungaji na mtoa pasi John Bocco walikuwa wameotea.
Mabao mengine yalifungwa na John Bocco ambaye alifunga hat trick yake ya kwanza ndani ya Simba ikiwa ni ya pili kwenye ligi kwa kuwa wa kwanza kufunga alikuwa ni Adam Adam wa JKT Tanzania na mengine yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili na Bernard Morrison alifunga bao moja.

Mgunda amesema:”Hakuna namna ya kufanya kwa kuwa matokeo yameshatokea siwezi kuyabadili na nimekubali nimepoteza hivyo makosa yaliyotokea tutayafanyia kazi.
“Tumefungwa kwa sababu ya makosa ya kujirudiarudia kwa wachezaji hasa kipindi cha kwanza tukafungwa mabao mengi ila angalau kipindi cha pili makosa yalipungua, tumefungwa kwa sababu ya makosa yetu hakuna namna tutafanyia kazi makosa, matokeo hatuwezi kuyabadili,” amesema.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Adelta
Simba kwa sasa wako vizuri
Elika
Hawana jipya wakubali walipigwa kifurushi inatosha
Lydia Emmanuel Magoti
Kwasimba nawakubali safu yao yaurinzi ipo vizuri Awana mpinzani wao yoyote yule kanyaga twende
Asia Abdy
Waendelee kufanya mazoezi huu sio mwisho Bali ni fundisho
Sarah
Simba wako vizuri nawanajitahidi sana
Caroline
Poleni costal
Fatuma kasomo
Safi cimba
aisha
Hamna timu hapo 7 majanga hayo
Sadick
Ushindi mno unasahaulisha uwekezezaji wa Mo wenye utata na hiki ndicho mashabiki wanataka kuona
Nasra
Sio kwa 7 hizo aisee
Theonestina
Pongezi ziende kwa cmba
Rehema
Sawa
Povel
Wamestail kipigo kile kitaka tifu Kwan Simba walikuwah kwny ubora wa Hali ya juu
Janeflora malisa
Safi sana mnyama
Hopemwaikuka
Dah! Mnyama katishaa sana
Saupha mohamed
Uyo ndo mnyamaa
Ester mmakasa
Simba oyeeee,kiukweli wamejuwa kunifurahisha sana.
Mwajumah
Waache kijitetea hawana jipya simba imejua kuifanya kazi
Fatina mfingi
Waache kujitetea hao
Angelina
Simba hana kazi mbovu
Ester jackson
Asante kwa jarida
Tatu
Simba mtu mbaya
magdalena
hawana la kujitetea kocha hakukinoa ipasavyo kikosi chake
Mariam mtandama
Safi sana
Sania
Simba imewakera majirani
Rahma
Simba ana mpenzan
Issa
Wagosi mlikosea wapi kuwaachia mikia
Sauda
Kichapo cha kibabe
warda
Kilikuwa kipigo mubashara