Mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy alitoa maelezo juu ya kesi yake ya ubakaji inayoendelea kusikilizwa mahakamni huko Uingereza, ambapo alisema kuwa ‘Najua mimi si Brad Pitt, lakini wanawake walikuja kwangu, si kwa sura yangu bali kwa sababu ya soka.’

 

Mendy: Wanawake Walikuja Kwangu si kwa Sura Yangu, Bali Kwa Sababu ya Soka

Beki huyo wa Manchester City aliliambia baraza la majaji kwamba wanawake walianza kumfuata akiwa na umri wa miaka 18 alipokuwa akiichezea Marseille katika ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa.

Lakini aliiambia mahakama ya Chester Crown Court ‘imekuwa mara kumi zaidi katika Man City ambayo ni moja ya timu bora Ulaya.’

Mendy, mwenye umri wa miaka 28, alianza kutoa ushahidi katika utetezi wake kwa msururu wa madai ya uhalifu wa ngono siku ya Jumapili ikiwa ni pamoja na ubakaji mara saba.

 

Mendy: Wanawake Walikuja Kwangu si kwa Sura Yangu, Bali Kwa Sababu ya Soka

Nyota huyo mwenye thamani ya paundi milioni 52, akiwa amevalia suti yake ya bluu, shati nyeupe na tai yenye muundo nyeusi na nyeupe, alikula kiapo kabla ya kujibu maswali ya wakili wake Eleanor Laws KC.

Alisema uhamisho wake wa paundi milioni 52 kutoka Monaco kwenda kwa mabingwa wa Premier League City mwaka wa 2017 ulikuwa ni kama ‘ndoto.’

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa alisema alienda kwenye vilabu vya usiku mara mbili au tatu kwa wiki baada ya kujiunga na City na kukutana na wanawake huko, ambao wengi wao walialikwa kurejea kwenye jumba lake la kifahari la The Spinney lililoko Prestbury, Cheshire, lenye thamani ya paundi milioni 4.7.

 

Mendy: Wanawake Walikuja Kwangu si kwa Sura Yangu, Bali Kwa Sababu ya Soka

Aliwaambia mahamakani kuwa: “Nilikuwa nikifurahia nyumba, nilikuwa nikifurahia wanawake. Nilifurahi sana kuwa hapa, nilifurahi sana. Nilifurahia soka pia”.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa