Kiungo wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Kalvin Phillips amejawa na matumaini kibao kabla ya kutajwa kwa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoiwakilisha nchi hiyo kwenye michuanno ya kombe la dunia nchini Qatar.

Kiungo huyo ambaye amekua akisumbuliwa na majeraha ya bega baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega lake wiki kadhaa nyuma, na sasa amesharejea mazoezini hivo kuamini anaweza kufanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha mwalimu Gareth Southgate.phillipsKiungo huyo aliehamia klabu ya Manchester City akitokea klabu ya Leeds United majira ya joto yaliyopita amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara huku mpaka sasa akiwa amecheza michezo 14 pekee kwenye michuano yote klabuni hapo.

Kocha Pep Guardiola amethibitisha kua Phillips ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi katika mchezo wa kombe la Carabao siku ya jumatano ambapo inaonesha kiungo huyo amepona maeraha yake na yuko tayari kucheza.

Kiungo Phillips anaweza kukosekana kwenye mchezo wa ufunguzi kati ya England na Iran lakini ana uwezekano mkubwa wa kujumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia kutokana kukosa utimamu wa michezo kadhaa.phillipsBado kiungo huyo ana imani ya kuitwa kwenye kikosi cha Uingereza japo pia hana uhakika sana kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Lakini wadau wengi wa soka na timu hiyo ya taifa wanaamini nafasi ya kiungo huyo bado ipo kutokana na kiwango alichokionesha kwenye michuano ya Euro 2020.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa