Aliyekuwa mkuu wa chama cha mpira wa miguu nchini Brazil 2012-2015 bwana Jose Maria Marin amehukumiwa jela miaka 4 baada ya kupatikana na hatia ya rushwa. Mkuu huyu mwenye umri wa miaka 86 alikuwa miungoni mwa maofisa 7 wa FIFA waliokamatwa mei 2015 katika hotel huko Zurich kwa madai ya rushwa.

Alihukumiwa na hakimu Pamela Chen katika mahakama iliyopo Blooklyn  akiwa ni ofisa wa kwanza kuhukumiwa kama sehemu ya  uchunguzi wa skendo ya rushwa ndani ya FIFA uliofanywa na marekani. Marin ambaye amewahi kuwa gavana wa Sao Paulo, mwaka uliopita alipatikana na na makosa 7 dhidi yake yanayohusiana na rushwa.

Marin anadaiwa kupokea rushwa kutoka kwa makampuni mbalimbali ya kutangaza michezo kama Copa America, mwanasheria wa Marin anadai kuwa watakata rufaa kwa hukumu hiyo.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa