Kompany Kuongeza Mda Manchester City

Kapteni wa Manchester City  Vincent Kompany  hafikirii kuiacha ligi ya Primier kwa sasa, anasisitiza hata katika umri wa miaka 32 bado anakuwa na uwezo wa kucheza kwa kiwango kikubwa. Kwa sasa anafurahia mpira wake kuliko mara nyingine yeyote huko nyuma. Kompany anadai licha ya kukwamishwa na majeraha lakini anaendelea vyema kila wakati.

Kompany amebakiza mwaka mmoja tuu ili amalize mkataba wake lakini anadai anao uhakika kuwa ataongeza mkataba mwingine,  mkataba wake katika klabu hiyo ulianza mwaka 2008. Kompany anasema kuna kitu watu wanashindwa kuelewa kuhusu yeye kwamba licha ya majeraha yake yeye bado ni mkimbiaji mzuri sana na bado anahisi kuwa na nguvu, ana pata nafuu zaidi na kujifunza vitu vingi zaidi kuhusu michezo kwa hali hiyo sio rahisi kwake kuacha premier.

 

2 Komentara

    Vicent yuko sahihi

    Jibu

    Visent akoseagi

    Jibu

Acha ujumbe