Real Madrid wameripotiwa kuwa wapo katika mchakato wa kufikiria uwezekano wa kufanya malipo ya euro milioni 35 kwa ajili ya kumrududisha James Rodriguez ambaye yupo kwa mkopo Bayern Munich. Mabingwa hawa walimruhusu Rodriguez kwenda Bayern kwa mkopo kwa kipindi cha miaka miwili, hivyo alitarajiwa kuwepo huko hadi mwaka 2019.
Hata hivyo inaripotiwa kuwa Real Madrid wameshindwa kumpata mbadala wa Christiano Ronaldo ambaye alijiunga Juventus kwa dau nono. Ronaldo ambaye mtiti wake ulikuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya Real ameacha pengo kubwa kwa klabu hii. Mabingwa hawa sasa wanajaribu kufikiria namna ya kuziba pengo lililochwa na Ronaldo huku wakipima kama ni sahihi kumfanya Rodriguez arudi kuziba hiyo nafasi.


Furahav
Itakua poa.