Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wameitawala tuzo hii kwa mda sasa. Mda unaenda haraka na kukaribia kupatikana mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or. Kaka, staa ambaye amewahi kuwa Real madrid ameondoa matumaini yake kwa Messi na Ronaldo kuwa ni washindani wa Ballon d’Or mwaka huu licha ya kutambua mchango wa wawili hao kwa timu zao katika soka.
Kaka ambaye ana umri wa miaka 36 anasema kwa sasa tuzo hiyo imepata ushindani mkubwa sana zaidi ya wawili hao baada ya kupatikana vijana wengine machachari katika ulimwengu wa soka. Japokuwa badhi ya wadau wa soka wanaamini huenda Ronaldo akaichukua tuzo hiyo mwaka huu kutokana na mafanikio waliyopata Real kwa mchango mkubwa wa Ronaldo, lakini Kaka amekuja na mpya na kuwataja watu wake ambao anaona wanafaa kuchukua tuzo hiyo.
Kaka anawataja Modric na Kylian Mbappe kuwa ndio wapinzani wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu kutokana na mafanikio makubwa waliyoyapata katika soka. Modric alikuwa ni sehemu ya Real Madrid waliopata ubingwa mara tatu mfululizo, lakini pia alipata mpira wa dhahabu katika fainali za kombe la dunia pale Urusi kutokana na mchango wake mkubwa katika timu ya Croatia. Lakini Mbappe pia amejitangazia kuwa kijana mwenye kipaji zaidi katika ulimwengu wa soka kufuatia tuzo aliyoipata katika fainali za kombe la dunia Urusi.


Mariam mtandama
Safi
Johnmary joel
Habari nzuri tunasubili kuona kama hata pata au la#meridianbetz
Povel
Messi hanapata hpo