Nyota wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi inaelezwa hajapokea ofa yeyote kutoka klabu ya Al Hilal ya nchini Saudia Arabia.

Klabu ya Al Hilal ilielezwa wiki moja nyuma kua wamefanya mazungumzo na Messi ili aweze kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia, Lakini imebainika taarifa hizo sio za kweli na mchezaji huyo hana mpango wa kuelekea nchini Saudia Arabia.MessiTaarifa kutoka klabu ya PSG zinaeleza nyota huyo ana mpango wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, Huku staa huyo akikaribia kusaini mkataba mpya utakaomuweka ndani ya timu hiyo kwa muda zaidi mbali na huu unaoisha mwisho wa msimu huu.

Ilitaarifiwa kua klabu ya Al Hilal ilipanga kumchukua staa huyo ili kuendeleza ushindani uliokuepo baina yake na gwiji anayekipiga kwa klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na klabu hiyo siku za hivi karibuni. Hivo klabu hiyo ingefanikiwa kumsajili Messi basi ingeweza kurudisha ushindani huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 11.MessiKlabu ya PSG inaelezwa kufikia hatua za mwisho kumpa mkataba mpya Lionel Messi ili aweze kusalia ndani ya klabu hiyo. Taarifa za ndani zinaeleza kua staa huyo pia yupo tayari kusalia ndani ya miamba hiyo ya Ufaransa klabu ya Paris Saint German.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa