Pogba Bado Anamvuto Sokoni?

Kuelekea usajili wa dirisha kubwa mwishoni mwa msimu huu, Paul Pogba ni mtihani. Bado anamvuto sokoni au ndio kwisha habari yake?

Pogba anaingia kwenye orodha ya wachezaji huru msimu huu ambao anamaliza mkataba wa miaka 5 na Manchester United. The Red Devils walimuekea mezani mkataba mpya toka mwezi Oktoba, 2021 lakini, mchezaji huyo hajausaini mpaka sasa.

Kwa upande wa United, inaaminika klabu hiyo haina mpango wa kuboresha mkataba huo kwa namna yeyote na, kama Pogba haoni sababu ya kuukubali basi ni dhahiri, yupo huru kuondoka baada ya msimu huu.

Swali ni, kama anaondoka, klabu gani inamuhitaji? Real Madrid walimtaka kwa sababu ni Zinedine Zidane ndiye aliyekua akimuhusudu. Sasa hivi, Madrid hawapo kwenye mchakato huo. Kule Turin, Juventus na Paul kuna muunganiko wa kipekee lakini, Maximilliano Allegri haonekani kuwa mwenye mpango na mchezaji huyo.

United ndio kabisa, hawajigusi, kama anasaini sawa kama hasaini sawa. Kule Camp Nou, ukata ni mkubwa. Hawana misuli ya kutaka kumsajili Pogba kutokana na matakwa yake ya kifedha.

PSG ndio klabu pekee inayohusishwa na mchezaji huyu ambaye, huenda akataka kurejea nyumbani (Ufaransa) baada ya kucheza nje ya nchi hiyo kwa muda mrefu (ngazi ya klabu). Ni kawaida kwa PSG kusajili wachezaji huru na kuwalipa mishahara mikubwa, pengine hili ndio chaka la Paul kama anaondoka United.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe