Pengine hili lilitegemewa kama ilivyo kwenye soka, LA Lakers imemuachisha kazi aliyekua kocha wao, Frank Vogel.
Vogel anaondolewa kwenye nafasi hiyo ambayo ameitumikia toka mwaka 2019 ambapo, alifanikiwa kuiongoza LA Lakers kwenye ubingwa wa NBA msimu wa 2019-2020. Msimu huu umekuwa ni shubiri kwa timu hii baada ya kuambulia vipigo 49 na hivyo kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kwenye nafasi ya 11.
Hakika huu sio uamuzi mrahisi kwenye uongozi wa timu hii ambayo, baada ya miaka 30, Vogel ndiye kocha pekee aliyeifanikisha timu hiyo kutwaa taji la NBA.
Tayari msimu huu umeisha kwa Lakers baada ya kushindwa kufuzu hatua ya Play-Offs, hii inamaanisha kuwa, uongozi wa timu hii unamuda wa kutosha kumtafuta mrithi wa Vogel.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.