Golikipa na kapteni wa timu ya Bayern Munich Manuel Neuer anaimani kuwa klabu yake iko tayari kuwakabili klabu ya Villarreal kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwenye mchezo wao wa pili
Manuel Neuer wakati akihojiwa alinukulia akisema, “nina furaha kwa ajiri ya mchezo wa kesho, hii ni ligi ya mabingwa, mara zote yamekuwa mashindano muhimu kwetu, tuna wachezaji wengi wadhoefu ambao wamecheza kwa muda mrefu.
Hatuna tatizo la uongozi, hilo halihitaji mjadala, tunazungumza sana na kufanya maboresho mara kwa mara, mawasiliano hapa ndio nyumbani.
Villarreal ni timu inayoshambulia vizuri sana, na kesho tutawaonyesha ubora wetu huku tukiwa na mashabiki wetu, mara nyingi tumekuwa hatuna mchezo mzuri kwenye hatua ya mtoano hasa mchezo wa kwanza kwenye klabu bingwa, tumekuwa tukipata matokeo yasiyo ridhisha, hatuogopi.”
Alipoulizwa kuhusu kocha wake Julian Nagelsmann kuhusu maandalizi ya kikosi Manuel Neuer alijibu, “Kocha amejidhatiti kwa ajiri ya mchezo, anajaribu kutuaanda kuwa bora kadri awezavyo, hususani kwenye mbinu za mchezo.”
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.