Sancho Aingia kwenye rada za PSG

Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho ameingia kwenye rada za mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa klabu ya PSG.

Klabu ya PSG inaelezwa inafukuzia saini ya Jadon Sancho na sio kwa mkopo kwani inaelezwa wametenga kitita cha kutosha kwajili ya kunasa huduma ya winga huyo ambaye alikua na msimu mzuri tangu ajiunge kwa mkopo klabu ya Borussia Dortmund msimu uliomalizika kitendo kilichowavutia mabingwa hao wa Ufaransa.sanchoKlabu ya Manchester United ilielezwa ipo tayari kumuuza winga huyo wa kimataifa wa Uingereza kama klabu inayomuhitaji itaweza kutoa dau ambalo wataridhishwa nalo, Kwani klabu ya Dortmund ilikua inamuhitaji kwa mkopo mchezaji huyo kwa mara nyingine japokua mshahara mkubwa anaochukua mchezaji imekua kikwazo.

Klabu ya PSG inamuona winga Sancho kama mbadala sahihi wa aliyekua mchezaji wao nyota aliyeondoka klabuni hapo na kutimkia klabu ya Real Madrid Kylian Mbappe, Hivo mpaka sasa klabu ya Man United inasubiria dau ambalo klabu ya PSG italiweka mezani kwajili ya kupata huduma ya mchezaji wao.

Acha ujumbe