Ac Milan Wanatarajia Leao, Giroud Kusaini Mkataba Mpya

Klabu ya Ac Milan wanatarajia kuwabakiza wachezaji wake wawili Rafael Leao na mshambuliaji Olivier Giroud ambao wachezaji hao wanakaribia kumaliza mikataba mwishoni mwa msimu huu.

Klabu ya Ac Milan imekua ikipambana kuwabakisha wachezaji wake muhimu ndani ya klabu kutokana na mipango ya muda mrefu ambayo wanayo klabu hiyo, Rafael Leao amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Giroud mkataba wake unamalizika ndani ya msimu huu.ac milanRafael Leao amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu hiyo kutokana na umuhimu ambao amekua nao ndani ya klabu hiyo, Lakini pia mshambuliaji Giroud amekua moja wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo mabingwa watetezi wa Serie A na ndio sababu klabu hiyo wanahitaji kuwabakiza wachezaji hao.

Klabu ya Ac Milan ipo kwenye kipindi ambacho inahitaji kujijenga zaidi na kurudi kwenye ubora wao ambao walikua nao miaka mingi iliyopita, Hivo klabu hiyo inahitaji kupata saini ya wachezaji wake ambao ni muhimu klabuni hapo ili kuendelea kujiimarisha zaidi.ac milanRafael Leao ni mchezaji anaefanya vizuri zaidi ndani ya klabu ya Ac Milan na kufanya vilabu mbalimbali barani ulaya kuhitaji saini ya mchezaji huyo kutokana na ubora wake, Hivo Rossoneri wanahitaji kupambana ili kuweza kumbakiza nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kwasababu upinzani ni mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.