Kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri amemmwagia misifa kibao kocha wa klabu ya Napoli Luciano Spalletti ambaye klabu yake inaongoza ligi kuu ya soka ya Italia.
Klabu ya Napoli ipo kwenye usukani wa ligi kuu nchini Italia huku wakiwa na alama saba mbele ya anayeshika nafasi ya pili ambao ni klabu ya Juventus. Huku Kocha Spalletti akiwa anapokea sifa nyingi kutokana na namna alivyoijenga timu hiyo.Kocha wa klabu ya Juventus Allegri amezungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya soka nchini humo dhidi ya vinara klabu ya Napoli siku ya ijumaaa. Na ndipo kocha huyo alipommwagia sifa kocha Spalletti na kusema licha ya kuongoza ligi kwa Napoli lakini kocha anapenda namna Spalletti anavyofundisha soka.
Klabu ya Juventus chini ya mwalimu Massilimiliano Allegri kesho atakabiliana na kocha mwenzake Luciano Spalletti, Katika mchezo huo unakua mtihani mzito zaidi kwa Juventus kwani wanashika nafasi ya pili wakiwa nyuma ya Napoli kwa alama saba hivo wakipoteza watakua wameachwa kwa alama kumi.Mchezo kati ya Klabu ya Juventus na Napoli utapigwa kesho ijumaa katika dimba la Allianz ambapo klabu ya Juventus wataua nyumbani ambapo Allegri akifanikiwa kupata matokeo mazuri dhidi ya Spalletti kesho basi itawapa nafasi klabu hiyo ya kuanza kuwaza ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.