Kocha wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Tottenham, Chelsea na Juventus Antonio Conte ameripotiwa kua kwenye rada za klabu ya Napoli mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Italia.
Antonio Conte ambaye aliachana klabu ya Tottenham Hotspurs amekua kwenye orodha ya makocha ambao wanatakiwa kuvaa viatu vya kocha wasasa wa klabu hiyo Rudi Garcia.Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham amekua hana timu baada ya kuachana na Spurs, Hivo ni wazi anaweza kujiunga na mabingwa hao watetezi nchini Italia kama kila kitu kitakwenda sawa.
Rais wa klabu ya Napoli yupo kwenye hatua za mwisho za kumvunjia mkataba kocha Rudi Garcia ikiwa ni kutokana na kocha huyo kua na mwanzo mbaya kunako ligi kuu ya Italia msimu huu jambo ambalo halileti picha nzuri kama mabingwa watetezi.Rais wa klabu ya Napoli alikiri walifanya makosa kumchukua kocha Rudi Garcia kutokana na kutokulijua soka la Italia vizuri, Lakini mpaka sasa wanafanya mazungumzo na Antonio Conte kutokana na kocha huyo kulijua soka la Italia vizuri na amewahi kutwaa vikombe kadhaa nchini humo.