Kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane ameweka wazi kua bado yupo nje ya uwanja kidogo kabla ya kurudi kutumikia klabu yeyote ile ikiwa ni baada ya kuulizwa atarudi lini uwanjani.

Kocha Zidane amesema kwasasa anafurahia maisha na familia yake na anasubiri kuangalia nini ambacho kitatokea mbeleni, Lakini kwasasa bado yupoyupo na ni wazi itahitaji muda bado kurudi dimbani.ZidaneKocha huyo wa zamani wa Real Madrid amekua akihusishwa mara kwa mara na timu mbalimbali kama kurejea Real Madrid, Lakini vilevile timu ya taifa ya Ufaransa lakini mpaka sasa haijafahamika kua kocha huyo ataifundisha klabu gani siku za usoni.

Kocha huyo amekua moja ya makocha wenye mafanikio kwa kipindi kifupi ndani ya klabu ya Real Madrid haswa baada ya kuweka historia ya kuchukua kombe la ligi ya mabingwa ulaya mara tatu mfululizo jambo ambalo halijawahi kufanywa na kocha yeyote.ZidaneZinedine Zidane aliongeza kwasasa tetsi zitakua nyingi sana kumhusu juu ya wapi ataelekea kwakua yeye ni meneja, Lakini akisisitiza watu wasubiri kuona ni wapi ataelekea muda ukifika kwakua yanayoongelewa yote kwasasa ni tetesi tu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa