Kiungo wa klabu ya klabu ya Juventus raia wa kimataifa wa Brazil Arthur Melo anatarajiwa kujiunga na klabu ya Fiorentina kwa mkopo wa msimu mmoja.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekua nje ya uwanja kwa takribani msimu mzima uliomalizika kutokana na majeraha ambayo yalikua yanamuandama mchezaji huyo akiwa kwenye klabu ya Liverpool.Kiungo Arthur Melo amekubali kujiunga na klabu ya Fiorentina ya nchini Italia ambapo anaona kama anaweza kurudisha ubora wake ambao alikua nao miaka kadhaa nyuma.
Kiungo Arthur Melo anatarajia kuchukua vipimo vya afya siku ya ijumaa ili kukamilsha dili lake la kujiunga na klabu ya Fiorentina, Huku kukiwa na kipengele cha klabu hiyo kumnunua jumla kwa dau la Euro milioni 20.