Winga wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane anatarajiwa kujiunga na klabu ya Al Nassr kutoka nchini Saudia Arabia kutokana na ripoti mbalimbali.

Taarifa mbalimbali zinaeleza kua Mane yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Al Nassr ili aweze kujiunga na klabu hiyo msimu ujao, Kwani winga wa klabu Chelsea Hakim Ziyech alifeli vipimo na klabu hiyo.ManeWinga huyo wa kimataifa wa Senegal hajafanikiwa kuonesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Bayern Munich mpaka kufikia kutaka kuachana na mchezaji huyo kutokana na kiwango chake.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Bayern zinaeleza kua Sadio Mane hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo hivo winga huyo kwasasa kwa upande wake anatafuta klabu ya kuichezea klabu kwa msimu ujao.ManeWinga Sadio Mane akifanikiwa kujiunga na klabu ya Al Nassr atakua miongoni mwa wachezaji wanaolipwa kiwango kikubwa cha pesa katika ligi kuu ya Saudia Arabia hivo kama mazungumzo yataende sawa atajiunga na klabu ya Al Nassr.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa