Bernardeschi Aelezea Anachotarajia Kutoka kwa Chiesa Akiwa Juve

Federico Bernardeschi amethibitisha kuwa angependa kurejea Juventus na kusisitiza kuwa watu wanapaswa kuzingatia kazi chafu ya Federico Chiesa badala ya kutarajia mabao na pasi za mabao katika kila mchezo.

 

Bernardeschi Aelezea Anachotarajia Kutoka kwa Chiesa Akiwa Juve

Winga huyo wa Toronto FC alizungumza na La Domenica Sportiva jana siku mbili baada ya ushindi wa 2-1 wa Juventus dhidi ya Monza.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Bernardeschi anatumia likizo nchini Italia kwani timu yake imeshindwa kufuzu kwa mechi za mchujo za MLS. Alitembelea uwanja wa mazoezi wa Juventus wiki iliyopita alipomwambia shabiki mmoja kwamba angependa kurejea Allianz Stadium katika dirisha la uhamisho la Januari.

Bernardeschi Aelezea Anachotarajia Kutoka kwa Chiesa Akiwa Juve

Winga huyo wa zamani wa Fiorentina alithibitisha hamu yake hiyo siku ya jana.

“Juventus iko moyoni mwangu, kipande cha moyo wangu bado kiko hapa, tuone, lakini ningefurahi kurudi,” alisema kama alivyonukuliwa na Ilbianconero.com.

Bernardeschi alicheza na Chiesa huko Fiorentina na Juventus na alizungumza kwa ufupi kuhusu mchezaji mwenzake wa zamani pia.

Bernardeschi Aelezea Anachotarajia Kutoka kwa Chiesa Akiwa Juve

Nilimwona akicheza michezo bora kwa Juventus, sio tu na timu ya taifa. Siku zote watu wanatarajia mabao au asisti, lakini wanapaswa kuzingatia zaidi kazi yake chafu.

Chiesa ana mabao manne na asisti mbili katika mechi 13 za Serie A msimu huu lakini amekuwa akicheza kama mshambuliaji wa kati huku kocha wa Italia Luciano Spalletti akimchezesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kama winga wa kushoto ambapo Chiesa anaonekana kuwa na ufanisi zaidi.

Acha ujumbe