Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na mshindi wa kombe la Dunia Fabio Cannavaro ameweka wazi ndoto yake ya kutaka kuinoa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Napoli.

Mshindi huyo wa kombe la Dunia mwaka 2006 ameapata uzoefu kwa kufundisha vilabu vya Asia na mashariki ya kati kama Al-Ahli, Guangzhou Evergrande, Al-Nassr, Quanjian Tianjin na kocha wa muda wa timu ya taifa ya China.

Cannavaro
Fabio Cannavaro

Alipohojiwa na Sky Sport Italia aliwambia, “mpira wa China unaweza kuchukuliwa ni wa ubora wa chini, lakini nimefundisha Guangzhou Evergrande, ambayo imechukua ubingwa mara tisa na makombe mawili ya ligi ya mabingwa Asia ndani ya miaka 10.

“Sitafanya makosa inapokuja swala la kuchagua timu ulaya, kwa hivi karibuni nimezungumza na Everton, Watford, Fiorentina na timu ya taifa Poland, lakini ndoto yangu ni kufundisha timu ya Italia.

Aliongezea Cannavaro, “nimesema tangu msimu kuanza kwamba napoli ni timu nzuri na wana kocha bora, Napoli itakuwa ndoto yangu, nimekuwa shabiki tokea nikiwa mdogo, najua nahitaji kufanya kwa juhudi kwanza na kuongeza uzoefu zaidi, tutaangali huko mbeleni nini kitatokea.” 


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa