Ibrahimovic: Theo Hernandez, Maignan, Leao Kubaki Milan

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Ac Milan Zlatan Ibrahimovic amesema wachezaji watatu klabuni hapo Theo Hernandez, Rafael Leao, pamoja Mike Maignan wataendelea kusalia ndani ya klabu ya Ac Milan.

Ibrahimovic amewataja wachezaji hao watatu ambao wamekua wanaonesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Ac Milan huku wakihusishwa na vilabu mbalimbali, Lakini gwiji huyo amesema hawaezi kuondoka klabuni hapo kwakua bado wana mikataba na klabu hiyo.IbrahimovicWachezaji Rafael Leao, Theo Hernandez, na golikipa Mike Maignan wamekua wachezaji wa Ac Milan ambao wanawindwa sana sokoni na vilabu mbalimbali barani ulaya, Jambo ambalo limemfanya gwiji Zlatan kuzungumza na kuweka kila kitu sawa kua wachezaji hao hawaezi kuondoka klabuni kutokana na kua na mikataba.

Alichokiongea gwiji huyo kina maana lakini kwenye mikataba ya wachezaji hao kuna vipengele ambavyo vimewekwa vya pesa kua timu itakayofika kiasi kilicho kwenye mkataba ni ruksa kwa mchezaji kuondoka, Hivo hali inaweza kuwafanya Milan kua wkwenye wakati mgumu.IbrahimovicMara kadhaa imeonekana wachezaji kadhaa wakisajiliwa kutoka klabu moja kwenda timu nyingine huku wakiwa na mikataba na timu walizopo, Hivo kwa kauli ya Ibrahimovic inaweza isifanye kazi kwakua licha ya wachezaji hao kua na mikataba lakini wanaweza kutimka klabuni hapo kama timu zitafika daul lililopo kwenye mikataba ya wachezaji hao.

 

Acha ujumbe