Bayern Munich Washusha Beki wa Kijapan

Makala iliyopita
Ibrahimovic: Theo Hernandez, Maignan, Leao Kubaki MilanMakala ijayo
Ligi Kuu Bara Kutumia VAR, Msimu Ujao
Beki Hiroki Ito mwenye umri wa miaka (25) amekua na msimu mzuri kwenye ligi kuu ya Ujerumani akiwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha VFB Stuttgart ambacho kimefanikiwa kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Ujerumani juu ya klabu ya Bayern Munich ambao walimaliza nafasi ya tatu.
Baada ya beki huyo wa kimataifa wa Japan kusajiliwa klabuni hapo hii inaonesha dhahiri kua tetesi zinazomhusu beki wa kimataifa wa Uholanzi De Ligt kutimka klabuni hapo zinaweza kutimia, Kwani beki aliyesajiliwa ni beki wa kati na De Ligt ni beki wa kati na amekua hapati nafasi ya mara kwa mara klabuni hapo.