Terzic Aachana na Borussia Dortmund
Makala iliyopita
Ederson Ana Furaha Atalanta, Licha ya Kuvutiwa na Liverpool
“Wapendwa Borussians, ingawa inaniuma sana sasa hivi, nataka kuwajulisha kuwa kuanzia leo, nitaondoka BVB. Ilikuwa heshima kubwa kuiongoza klabu hii kuu hadi kwenye ushindi wa DFB-Pokal na hivi karibuni kufika kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.”
Kocha Terzic akiitumikia klabu hiyo kama kocha mkuu kwa misimu miwili amefanikiwa kubeba taji la DFB Pokal na kuifikisha klabu hiyo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu ulimalizika ambapo walipoteza kwa mabao mawili kwa bila mbele ya Real Madrid, Huku akiwa kocha wa kwanza kuipeleka Dortmund fainali ya ulaya baada ya miaka 10.