Makocha wa Italia Waweka Historia Kwenye Ligi ya Mabingwa

Ilikuwa hatua nzuri ya makundi kwa makocha wa Italia katika Ligi ya Mabingwa, huku makocha hao wakipeleka timu zao katika hatua ya mtoano ambayo ni 16 bora.

 

Makocha wa Italia Waweka Historia Kwenye Ligi ya Mabingwa

Wawakilishi watatu kati ya wanne wa Serie A katika kinyang’anyiro hicho walitinga hatua ya 16 bora. Napoli, Milan na Inter zote zitashiriki katika hatua ya mtoano, huku Juventus pekee wakishindwa kutinga hatua inayofuata kufuatia kampeni yao mbaya Ulaya.

Makocha watano wa Italia wamefuzu hadi hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa katika msimu mmoja kwa mara ya kwanza kabisa. Real Madrid ya Carlo Ancelotti, Tottenham ya Antonio Conte, Napoli ya Luciano Spalletti, Milan ya Stefano Pioli na Inter ya Simone Inzaghi zote zitachuana katika hatua ya mtoano.

Makocha wa Italia Waweka Historia Kwenye Ligi ya Mabingwa

Massimiliano Allegri atakuwa amechanganyikiwa kutokana na timu yake ya Juventus kushuka kwenye Ligi ya Europa. Sasa wanasubiri kuona ni timu gani watakutana nayo kwenye mechi ya mtoano.

Droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa itafanyika Jumatatu Novemba 7 saa 11.00 kwa saa za Uingereza.

Acha ujumbe