Mchezo mkali kati ya klabu ya As Roma ambao watakua nyumbani Estadio de Olimpico kuwakaribisha Napoli utapigwa usiku wa leo katika ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A.romaMchezo unatarajiwa kua mkali sana kutokana uwezo wa timu zote mbili kwasasa ambapo klabu ya Napoli haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini humo ambapo kiyu ambacho kinafanya mchezo huo kua wakuvutia zaidi kwani Roma wanaonekana kua kwenye kiwango kizuri kwasasa.

Swali kubwa leo ni je vijana wa Jose Mourinho wanaweza kufuta rekodi ya vijana wa Luciano Spalletti ambao wamekua na rekodi nzuri sana msimu huu kwenye michuano yote waliyocheza huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.romaRoma watakua na nafasi ya kusimamisha rekodi ya kutokufungwa msimu huu kwenye ligi hiyo na mashindano yote huku klabu hiyo wakipata nafasi ya kusogea juu zaidi kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Mchezo huo unakwenda kuwakutanisha makocha wenye ubora mkubwa kunako ligi kuu nchini Italia na mechi ikitegemewa kua na ushindani mkubwa kutoka na ubora wa timu hizo pamoja na benchi la ufundi ambapo kuna makocha bora.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa