Napoli Haina Mpango wa Kumuachia Kvaratskhelia

Klabu ya Napoli chini ya Rais wa klabu hiyo Aurielo De Laurentiis imeweka wazi haina mpango wa kumuachia nyota wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia.

Rais wa klabu hiyo De Laurentiis inaelezwa leo amekutana na winga Kvaratskhelia na wakala wake kufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwajili ya kujaribu kufanya ushawishi wa kumbakiza mchezjai huyo ndani ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao wa 2024/25.napoliTaarifa zinaeleza kua winga huyo ana mpango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo msimu ujao kwajili ya kutafuta changamoto nyingine nje ya klabu hiyo, Lakini klabu hiyo inaelezwa haiko tayari kumuachia mchezaji huyo ambaye anafanya vizuri na timu yake ya taifa ya Georgia.

Mpango wa klabu ya Napoli uko wazi ni kumbakiza mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo kwakua bado ana mkataba ndani ya klabu mpaka mwaka 2027, Lakini inaelezwa kua pamoja na kua na mkataba ndani ya timu hiyo lakini timu hiyo ina uwezekano wa kumuongezea mkataba mwingine baada ya michuano ya Euro 2024.napoliKocha mpya wa klabu hiyo Antonio Conte ameweka wazi anatamani kufanya kazi na winga Kvaratskhelia kueleka msimu ujao na akimuona kama mchezaji muhimu kwenye mipango yake ya msimu ujao, Lakini bado kuna uwalakini kwa mchezaji kama atakubali kubaki ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe