Osimhen: Ninapambana Ili Niweze Kucheza Epl

Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria anayekipiga klabu ya Napoli ya nchini Italia Victor Osimhen amesema anapambana kila siku ili kuhakikisha anacheza kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Victor Osimhen ana ndoto kubwa ya kucheza ligi kuu ya Uingereza licha ya kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya Italia Serie A, Mshambuliaji huyo mpaka sasa anafanya vizuri sana ndani ya klabu ya Napoli akiwa mfungaji bora wa ligi kuu nchini humo mpaka sasa.osimhenMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria amezungumza na wanahabari na kusema ” Ninapambana kila siku ili kuhakikisha ninatimiza ndoto yangu ya kucheza ligi kuu ya Uingereza,Ninataka kuendelea na kiwango ninachokionesha kwasasa, Serie A ni moja ya ligi tano bora ulaya ni hisia ya ya kushangaza sana kwangu”

Vilabu mbalimbali barani ulaya vinafatilia kwa karibu kupata saini ya mshambuliaji Victor Osimhen kutokana na kiwango bora ambacho amekua akikionesha ndani ya klabu ya Napoli, Huku klabu ya Napoli ikiwa inatarajia kupokea pesa nyingi ya usajili kupitia mchezaji huyo.osimhenKlabu ya Manchester United inatajwa kuwania saini ya mshambuliaji Osimhen kwa karibu zaidi kwakua klabu hiyo imekua na shida katika safu yake ya ushambuliaji, Ndio sababu ambayo inafanya miamba hiyo ya soka nchini Uingereza kuhusishwa zaidi na mshambuliaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.