Sky Sport Italia inadai kuwa jeraha la goti la Paulo Dybala si baya kama ilivyodhaniwa awali na mshambuliaji huyo wa Roma na Argentina hatahitaji kufanyiwa upasuaji.
Roma walihofia Dybala angekaa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kumuona La Joya akitoka uwanjani akilia wakati wa ushindi wa 4-1 dhidi ya Cagliari hapo jana, kutokana na jeraha linaloshukiwa kuwa la goti.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Hata hivyo, Sky Sport Italia inaripoti suala la kimwili la Dybala si kubwa kama ilivyofikiriwa hapo awali.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alifanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Villa Stuart usiku kucha na vipimo viliondoa kupasuka kwa mishipa au jeraha ambalo lingemlazimu Muajentina huyo kutocheza kwa muda mrefu.
Kulingana na ripoti hiyo, Dybala anaweza hata kurejea uwanjani baada ya mapumziko. Hakika, hatahitaji kufanyiwa upasuaji wa goti. Kulingana na Gazzetta, lengo la Dybala ni kurejea kwa mechi ya ugenini huko Inter mnamo Oktoba 22.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Roma watakuwa wenyeji wa Monza ya Raffaele Palladino kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico Jumapili, Oktoba 22, katika mchezo wa kwanza wa Serie A baada ya mapumziko ya Oktoba.