Baada ya mapumziko ili kupisha michezo ya kimataifa ya EURO 2020 kwa sasa ligi hiyo inarudi kwenye kasi yake ya awali huku ikiwa ni safari ya kuelekea kuhitimisha ikiwa ni michezo kadhaa tu inayohesabika iliyosalia ili kumalizika kwa ligi hiyo msimu huu. Kurejea kwa ligi hiyo bado kunashuhudia ushindani mkubwa na wa aina yake.
Kama ilivyo ada nafasi ya juu bado ina ushindani mkubwa mbele ya Liverpool na Man City huku nafasi nyingine kati ya Chelsea, Arsenal na Man United zikiwa zinagombaniwa kwa upekee zaidi kutokana na tofauti ya alama iliyopo kati ya klabu hizo ambapo kila mmoja ana nafasi kubwa ya ama kupanda juu zaidi endapo ataendelea kushinda au kushuka endapo atapoteza michezo yake.
Baadhi ya mechi zitakazoshuhudiwa leo kwa upinzani mkubwa ni kati ya Manchester United na Watford ambapo kwa siku za hivi karibuni Watford wamekuwa wakiwasumbua kwa kiwango kikubwa wakubwa wengi wa ligi hiyo kutokana na uiamara wao wa safu ya ulinzi ambayo inajitahidi kuzuia mipira mingi ya hatari kupenya kwenye lango lao na ni jambo ambalo litaifanya mechi hiyo kuwa ngumu baina ya pande hizo mbili.
Fulham na Manchester City ni kati ya mechi zitakazochezwa lakini kwa upande mwingine tunaweza kusema mshindi wa mechi hiyo tayari anajulikana kutokana na kasi ya City na kuhitaji kwake matokeo ili aendelee kumuongoza Liverpool kwa tofauti ya alama. Hivyo mechi hiyo inampa nafasi ya kuendelea kusonga mbele bila upinzani.
Brighton watamkaribisha Southampton kwenye uwanja wao japo mwenyeji huyo hajawa na mwenendo mzuri na wote wanaenda kukutana wakiwa na uhitaji wa alama hivyo ni mechi itakayotawaliwa na faulo za kutosha na idadi ndogo ya magoli kwa mwonekano wa mechi itakavyokuwa. Hivyo, kwa jicho la pekee itakuwa ni mechi ngumu sana.
Burnley na Wolves kwa upande mwingine tunaweza kusema mechi hii lazima iegemee upande mmoja kutokana na uwezo wa Wolves kwenye ligi hiyo. Wamekuwa kikwazo hata kwa klabu nyingine kuondoka na matokeo mbele yao. Inakumbukwa kwamba ndiyo waliomtoa United kwenye michuano iliyokuwa inaendelea hivyo ni shughuli pevu kwao.
Leicester City mbele ya AFC Bournemouth hii nayo ni mechi ngumu kati ya wawili hao kutokana na historia zao. Pamoja na kuwa Leicester hajawa na msimu mzuri lakini anapewa asilimia nyingi za kuchukua alama kwenye mchezo huo. Wana kila sababu ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki zao wanaotegemea makubwa kwao.
West Ham United watakuwa wanaumana na Everton baada ya ushindi mbele ya Chelsea wanaingia uwanjani wakiwa ugenini kupambana na Wagonga Nyundo wa Jiji hilo. Ushindi huo wa awali mbele ya Chelsea unaweza kugeuka kama hamasa kwao kuchukua alama kwa wenyeji hao. Pia, mechi nyingine itakuwa kati ya Palace dhidi ya Huddersfield Town.


Povel
Habar njema