Real Madrid wanaripotiwa kujiandaa kuweka kitita cha £125m kumuwinda staa wa Manchester United Paul Pogba ambaye hivi karibuni alionekana kuiweka wazi ndoto yaje ya kuchezea Real Madrid.
Kwa mujibu wa The Sun, Real Madrid walivutiwa na staa huyo kutaja kuwa Real Madrid ni ndoto ya mastaa wengi huku na yeye akiwemo miungoni, hii ilionekana wazi kuwa ni nia ya kutaka kuungana na Zinedine Zidane siku moja pale Real Madrid.
Pogba alirejea Manchester United akitokea Juventus kwa ada ya paundi milioni 86, dau lililovunja rekodi ya dunia kwa wakati wake. Dau la staa huyu kwa sasa limepanda na Real wako tayari kuweka mezani kitita cha paundi milioni 125 kumfanya nyota huyu atue pale United.
Hata hivyo ripoti zinadai kuwa itawagharimu Real zaidi ya paundi milioni 125 kumnasa staa huyu huku Manchester United mara kadhaa wakionekana kusisitiza kuwa staa huyu hauzwi kwa dau lolote lile.
“Kama ninavyosema mara zote, Real Madrid ni ndoto ya kila mtu. Ni moja kati ya klabu kubwa zaidi duniani. Pia kuna Zidane kama kocha na ni ndoto ya yeyote ambaye anapenda soka. Kwa sasa niko Manchester United. Hakuna anayejua kesho itakuwa vipi. Niko Manchester United na ninafurahia kuwa hapa.” – Paul Pogba


Povel
Habar njema