Messi Akamata Nafasi ya 1, 2 na 3 kwa Pamoja!

Fundi wa soka kutoka Barcelona Lionel Messi amebamba nafasi 3 kwa pamoja kwenye goli bora zaidi katika historia ya Barcelona. Messi amechapa jumla ya magoli 591 kwenye gemu 673 alizocheza.

Nyota huyu amekamata nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu kwenye kura zilizopigwa na wadau juu ya goli bora zaidi kwenye historia ya soka kabuni hapo. Jumla ya kura zilizopigwa ni zaidi ya laki 5 kutoka nchi zaidi ya 160.

Goli alilolichapa mwaka 2006-07, kwenye fainali ya Copa del Rey dhidi ya Getafe baada ya kuwapita walinzi wanne na kumchambua golikipa, ndiyo limeibuka kuwa goli bora zaidi kwenye historia yaklabu hiyo. Goli hili lilikusanya asilimia 45 ya kura.

Goli jingine lililokuwa ni jitihada za Messi mwenyewe kwenye gemu dhidi ya Athletic Bilbao katika fainali ya Copa del Rey limechukua asilimia 28 ya kura na kuwa nafasi ya pili. Goli lililoshika nafasi ya tatu ni goli alilochapa dhidi ya Real Madrid msimu wa mwaka 2010-11 pale Santiago Bernabeu likipata kura asilimia 16.

Nafasi ya 4 imekamatiwa na goli la Sergi Roberto la dakika za mwisho kabisa kwenye gemu dhidi ya PSG mwaka 2017, goli lililowasaidia Barca kupata tiketi ya kuingia kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.