Messi: Nimemkumbuka Ronaldo

Uwepo wa mchezaji fulani huchochea kwa kiwango kikubwa ari ya mchezaji mwingine kiushindani na hata kimataji. Messi ameweka wazi kwamba sio siri tena kwake amekumbuka kwa kiwango kikubwa uwepo wa Ronaldo kwenye ligi kutokana na wawili hao kwa pamoja kuweka historia kubwa kwenye ligi hiyo.

Baada ya kuwasaidia Madrid kushinda taji la nne la klabu bingwa Ulaya, nyota huyo alitimkia zake Serie A kujiunga na miamba wengine wa soka, Juventus. Lakini pamoja na kutimka ndani ya ligi hiyo hakuna kilichopungua kwake kwa sababu anaendekea kufunga kama kawaida na ubora wake bado upo juu kama kawaida.

Amedhihirisha hilo baada ya kuwaadhibu goli tatu Atletico katika mchezo wao wa kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Akiwa amewafunga kwa kusawazisha makosa waliyoyafanya awali kwenye mechi yao ya utangulizi. Lakini wakiwa nyumbani mchezaji huyo aliwarudisha Juventus mchezoni kama ilivyo kawaida yake.

Lakini upangaji wa pacha unaonesha kabisa kwamba wawili hao hawana nafasi ya kukutana kabisa katika hatua yao ya mwanzo labda ikitokea wamekutana hatua ya fainali kwenye michuano hiyo. Na hilo linategemeana kama wote wataweza kuruka mashimo waliyotegewa njiani kuelekea fainali.

Madrid kwa sasa wanajikongoja alama 12 nyuma ya kinara wa ligi, Barcelona na Messi ameliona hilo kwa kusema kwamba anakumbuka sana uwepo wa Ronaldo kwa sababu aliifanya La Liga kuwa kitu cha kipekee sana na ilikuwa kwenye mvuto kutokana na ushindani baina yao japo ilikuwa changamoto kupata mataji kwa urahisi.

Messi: Nimemkumbuka Ronaldo

Kwake Juventus bado ni klabu sahihi kwa Ronaldo na kutokana na mechi aliyoicheza dhidi ya Atletico ni dhahiri kwamba hakuna anayeweza kuwachukulia kwa kiwango cha kawaida maana bado wana kikosi kigumu chenye wachezaji wazuri na wenye nidhamu ya kujua nini kinahitajika ili klabu ipate heshima kubwa.

Wawili hao ni miongoni mwa wachezaji ambao wameweka historia kubwa kwenye soka na kila mmoja ameweka historia ya aina yake. Hili linaonekana wazi na halina kificho kabisa. Japo Messi hajataka kuwasahau wachezaji wengine wa kikosi chake wakiwemo Luis Suarez kwamba nao wana nafasi ya juu kwa wanayochangia kiushindani kwenye ligi hiyo.

Wachezaji wengine ambao Messi anawaona bado wana mchango mkubwa kwake na mbele ya soka ni Neymar, Mbappe, Hazard na Sergio Arguero. Na amesikitishwa sana kukosekana kwa mchezaji huyo katika kikosi cha timu ya taifa kwa kudai kwamba nyota huyo ni mchezaji wa pekee sana kwenye kikosi chao na anahitaji kupewa nafasi kikosini huko ili kuifanya timu ya taifa lake kuwa imara zaidi.

Makala iliyopita

2 Komentara

    Ukifanya kitu kizuri lazima ukumbukwe maana historia hudumu daima

    Jibu

    Lazma utamkumbuka sana.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.