Marouane Fellain Ametangaza Kustaafu

 

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Marouane Fellain ametangaza kustaafu soka la kimataifa. Mwanasoka huyu ameweka wazi kuwa kwa sasa hatakuwa mchezaji wa kimataifa wa Belgium.

Staa huyu alikamilisha usajili wake kwenye klabu ya China akitokea Chelosea mwezi uliopita ametangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa soka lake kama mchezaji wa Ubelgiji limefika tamati.

Nyota huyu ambaye bana umri wa miaka 31 alikuwa ni mmoja wa wacheaji ambao walikuwa kwenye kikosi kilichoenda kupambana kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia kule Urusi.

Marouane fellain Ametangaza Kustaafu

Fellain kabla ya kutangaza kustaafu aliitwa kwenye kikosi cha taifa hilo kwenye mechi 87 na amefanikiwa kufunga magoli 18 toka alivyoanza rasmi kucheza soka la kimataifa mwaka 2007.

“Baada ya miaka 12 ya kuiwakilisha Ubelgiji katika ngazi kubwa zaidi, nimeamua kustaafu soka la kimataifa. Halijawa suala rahisi kwangu kufanya maamuzi haya lakini nahisi wakati sahihi wa mimi kuachia ngazi umefika ili kuruhusu kizazi kipya cha Wabelgiji kuendeleza kipindi hiki muhimu cga mafanikio ya soka la Ubelgiji.”

Staa huyu pia amegusia baadhi ya vipindi ambavyo alifurahia kazi yake ya mpira toka alipoanza wakati akiwa na Mashetani Wekundu, na anajivunia kuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia.

Anawashukuru wote aliokuwa nao kwenye kazi yake ya soka akiwa anashiriki michezo yote ya kimataifa, ambao kwa namna moja au nyingine walitoa mchango chanya kwenye mafanikio ya kipindi chake.

 

Acha ujumbe