Mbio za Barca na Real kwa Skriniar

Real Madrid na Barcelona wanataka kumsajili Milan Skriniar wa pale Inter Milan. Kwa mujibu wa wakala Mithat Halis, yeyote kati ya Barca na Real anaweza kumnasa staa huyu.

Skriniar alitimba Inter Milan akichomokea Sampodoria mwaka 2017 na amefanikiwa kuwa mmoja wa walinzi bora kabisa duniani kwa nafasi yake.

Staa huyu mwenye miaka 24 amekuwa akihusishwa na mabingwa wa Real Madrid Manchester United, lakini anaweza kuungana na Real Madrid au Barcelona mwisho wa msimu huu.

“Real Madrid wanataka kumsajili, hata Barcelona pia. Kama wataweza kuwashawishi Inter wanaweza kumsajili msimu huu wa joto” -Mithat Halis

Skriniar amekuwa mchezaji muhimu anayewavutia klabu nyingi kubwa ulaya kwa sasa. Amecheza gemu 25 kwa Serie A, amefikisha jumla ya gemu 33 kwa michuano yote. Hadi msimu huu unafika tamati itafahamika kama ni Barca au Real wamemnasa!

2 Komentara

    Habari njema kwa mashabik#meridianbettz

    Jibu

    Skrianiar Yuko vizuri sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.