Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United Wyne Rooney anasema kuwa yeye anaona hakuna mtu yeyote mwingine anayefaa kupewa nafasi ya umeneja wa kudumu klabuni United zaidi Ole Gunnar Solskjaer.
Solskjaer ameweza kurejesha klabu ya Manchester United kwenye fomu na kuwapa morali zaidi toka alipochukua kibarua klabuni hapo ambacho mkataba wake unatakiwa uishe mwisho wa msimu huu.
Uongozi wa klabu ya Manchester United walinukuliwa wakisema kuwa wao hawana haraka ya kufanya maamuzi ya mrithi wa kudumu wa umeneja klabuni hapo, lakini bila shaka kazi ya ole Gunnar imerejesha amani kwa wakuu hawa kwa klipindi cha mda mfupi.
Licha ya kuwa tangazo rasmi la nani atakuwa meneja wa kudumu wa Mashetani Wekundu, huku meneja wa Spurs Mauricio Pochettino naue akihusishwa na kibarua hicho, Rooney anasisitiza kuwa hapana shaka Ole Gunnar ndiye pekee anayestahili.


Furahav
Nikwel mana yuko vizuri.