Nyota wa UFC, McGregor amemzungumzia Ronaldo kutokana na historia yake na aina ya matokeo anayoleta kwenye soka na zao analolitoa katika klabu yake mpya ya Juventus kwamba ni mchezaji ambaye sio tu anacheza soka lakini pia amewekeza nguvu zake na uwezo wake katika soka na ana nidhamu kubwa sana kwenye soka.
McGregor ambaye pekee anaonekana kuwa ni mchezaji mwenye uwezo kwa kuweza kunyanyua mataji mawili ya UFC mfululizo hajapata kuzungumziwa sana kwenye historia pamoja na mafanikio hayo makubwa. Sio mtu anayepigiwa sana upatu pamoja na uwezo wake kuwa wa kipekee hasa kwenye ulingo na nje ya maisha yake ya kawaida.
Mchezaji huyo alipokuwa akihojiwa alizungumzia maisha yake ya ulingoni na kujaribu kujilinganisha ubora wake na nyota wa LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovich ya kwamba mwanasoka huyo kwa sasa anataka kuwa McGregor wa soka. Japo nyota huyo alishindwa kabisa kuficha uhalisia wa namna anavyomkubali Ronaldo kwa kile anachokifanya.
Hakuna mwenye kubisha uwezo wa Ronaldo kwa kuhitaji afanye jingine kwa sasa maana amelifanyia soka kila kitu pamoja na kwamba kuna vikombe hajaweza kushinda; hilo ni jambo dogo la kibinadamu kwani katika maisha huwezi kushinda mitihani yote. Lakini aliyoyafanya ni makubwa na yanafaa kufunzwa hata kwa kizazi kijacho cha soka.
Uwezo wake mkubwa aliouonesha mbele ya Atletico katika mechi yake ya michuano ya klabu bingwa Ulaya na kufanikiwa kuipeleka klabu yake hiyo kwenye robo fainali ya michuano hiyo ni jambo la pekee linalohitaji pongezi za kila aina na ni miongoni mwa mambo ambayo nyota hiyo wa UFC amejaribu kuyazungumzia.

Ameendelea kumsifia mchezaji huyo kwa kujaribu kuhusianisha umri wake na mambo ambayo anayafanya. Kwa umri wa miaka 34 na vitu anavyovifanya unaweza kumlinganisha na wachezaji wa miaka 20 kama Mbappe lakini umri wake umesogea sana lakini bado ujuzi wake hauonekani kabisa kushuka wala kupotea anazidi kupandisha makali kadri siku zinavosonga.
McGregor amekuwa shabiki mkubwa wa United kwa miaka kadhaa na anasema mapenzi yake ndani ya klabu hiyo ni makubwa na hategemei kuacha kuishabikia klabu hiyo kwa sababu ya historia aliyonayo ndani ya klabu hiyo na bado anakumbuka United ya Ronaldo chini ya Fergie miaka ya nyuma na bado anavutiwa sana na klabu hiyo.
Kwa sasa anaendelea kuwapa moyo wachezaji walio ndani ya kikosi hicho kuwa hawana budi kupambana ndani ya kikosi hicho ili kujijengea heshima kubwa ambayo itakuwa msaada kwa kizazi chenye mapenzi na klabu hiyo. Anavutiwa na uwezo wa Pogba na Rashford kwamba anawaona kwenye ramani ya soka zuri chini ya Ole Gunnar Solskjaer na anawataka kuongeza jitihada zaidi maana kikosi hicho kipo kwenye mikono yao.


Johnmary joel
Nikweli kabisa ronaldo ananidham sana na ndiyo maana anafanikiwa#meridianbettz
Issa
Ni safi
aisha
Big up kwa ronaldo