Huenda kampeni ya kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya EURO 2020 ikaanza bila ya baadhi ya nyota katika vikosi vya baadhi ya timu za taifa kutokana na majeraha ya baadhi ya wachezaji na pia kukosekana kwa baadhi ya wachezaji mazoezini aidha kwa kuchelewa kuripoti kutokana na majukumu ya klabu pia wengine kujiondoa kabisa katika ushiriki huo.
Nyota wa United, Marcus Rashford huenda akakosekana katika mechi zake za awali za michuano hiyo ya Euro kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata hivi karibuni. Majeraha hayo yameweza kumuweka nje ya michuano hiyo kwenye mechi za mwanzo zote wanapotafuta tiketi ya mapema; ikiwemo ile kati yao na Jamhuri ya Czech.
Tatizo hilo limetokea baada ya kushindwa kuungana na timu yake kufanya mazoezi ya mwisho ambayo yana umuhimu sana katika kujua ushiriki wa kila mchezaji ambaye amepewa majukumu ndani ya kikosi hicho. Hadi sasa jumla ya wachezaji 21 wameidhinishwa tayari kuonesha ushiriki wao kwenye kampeni hiyo ya kutafuta nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo.
Idadi hiyo sio ile iliyokuwa imehusishwa hapo mwanzo ambapo imepungua kutokana na majeraha ya Rashford ambayo yanamfanya akae nje na kuwapa nafasi wengine waweze kuonesha uwezo wao bila uwepo wa nyota kama hawa. Japo hili linaweza lisilete shida kwa taifa hilo kutokana na kuwa na wachezaji wengi ambao watakuwa mbadala.
Kwa taarifa za awali ni kwamba Rashford hatoweza kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kutokana na majeraha hayo ambayo yanamfanya aonekane mguu ndani, mguu nje kwenye michuano hiyo na hata akipata ahueni hawezi kurudi uwanjani; kutokana na hali hiyo ataendelea kusalia nje ya kikosi. Japo ilisadikika kwamba angeweza kurejea baada ya mechi yao na Czech lakini kwa sasa hataweza hata akiwa vizuri; pia hatoweza kuonesha ushiriki wake kwenye mechi dhidi ya Montenegro.

Majeraha hayo yanaweza kuwa na maumivu kwa United ambao kwa sasa wanaangalia namna ya kukujikusanyia alama katika michuano wanayoshiriki. Kukosa huduma za mchezaji kama huyu ni jambo ambalo lazima lisababishe ugumu kwa klabu kuelewa kwa urahisi mazingira ambapo wanakosa huduma ya mchezaji ambaye ni tegemezi kwenye kikosi huku wakikabiliwa na mechi dhidi ya Watford wakirudi kwenye ligi.
Anthony Martial na Romelu Lukaku hadi sasa hawatakuwepo ndani ya vikosi vya kimataifa jambo ambalo linaweza kuwashtua sana United. Martial hataweza kuwa na kikosi chake cha Ufaransa na Ubelgiji wao watamkosa mchezaji huyo kwenye mechi zao kutokana na kukumbwa na majeraha ambayo yanaendelea kumuandama.
Hili linaweza kuwa janga kwa tiku za taifa lakini janga zaidi kwa klabu inayomiliki wachezaji hao na hicho kikosi kipo kwenye kampeni za kukusanya alama ili kuendelea kuleta ushindani kwenye nafasi nne za juu.


Furahav
Hatari sana.
Povel
Gud news