Baada ya makundi ya robo fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kupangwa na baadhi ya klabu kukutana katika mechi zinazotegemewa kuwa ni ngumu na zenye kuvutia ambazo ni kati ya United na Barcelona; mechi hiyo imekuwa na upekee mkubwa sana na imekuwa ikizungumziwa na wengi sana mitandaoni.
Wengi wanamwona kama United ni mnyonge sana mbele ya Barcelona katika mechi hiyo. Wakiamini kwamba hana nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo jambo ambalo kuliangalia kwa nguvu ya soka na uwezo wa United katika siku za usoni lolote linaweza kutokea pamoja na kuwa watacheza na miongoni mwa klabu bora kabisa duniani. Leo tumekurudisha kipindi cha nyuma kidogo kuangalia historia za wawili hawa:
Kipindi cha nyuma kidogo miaka ya 1984 United walikuwa na uwezo wa kumfunga yeyote kutokana na uwezo wao wa wachezaji aliokuwa nao kwa kipindi hicho. Uwezo wa Bryan Robson ulikuwa unawapa nguvu United kutokana na aina ya kiwango chake na uwezo aliokuwa nao uwanjani kuweza kuipa timu matokeo chanya. Pia, alikutana na Barcelona katika kombe hilo lililokuwa maarufu kwa jina la European Cup Winners’ Cup hatua ya robo fainali.

Mwaka 1991 walikutana katika mechi yao na Barcelona katika michuano mikubwa inayoendana na hiyo iliyojulikana kama European Cup Winners’ Cup kwenye hatua ya fainali na United kuibuka kidedea kwenye michuano hiyo na kujijengea historia mbele ya miamba hao wa soka Hispania.
Mwaka 1994 walikutana kwenye hatua ya makundi ndani ya michuano hiyo ambapo matokeo ya mechi hiyo yalikuwa 2-2 huku wawili hao wakitoshelezana nguvu ndani ya mechi hiyo. Ikishuhudiwa na uwezo mkubwa uliooneshwa na wachezaji kama Roy Keane, Ryan Giggs, Denis Irwin, Eric Cantona, Andrei Kanchelskis, Peter Schmeichel, Ryan Giggs, Brian McClair na Mark Hughes.
Mwaka 1998 walikutana tena ndani ya michuano hiyo kwenye hatua ya makundi huku ikishuhudiwa timu hizo zikimaliza mchezo wao kwa kutoshelezana nguvu kutokana na kuibuka na sare ya 3-3 baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Dwight Yorke na Andy Cole.
Pia, mwaka 2008 walikutana katika hatua ya nusu fainali kwenye hatua ya marejeano United wakifanikiwa kupata ushindi wa 1-0 mbele ya Barcelona. Kwa kipindi hicho timu zote zilikuwa na vikosi vya aina yake huku Barcelona ikiwa na watu kama Lionel Messi, Xavi, Andres Iniesta na Samuel Eto’o. Lakini walilala kwa goli la Paul Scholes.
Siku zote soka ni mchezo wa matokeo ambapo inategemeana na nguvu ya kikosi katika siku husika. Kuna uwezekano mkubwa kwa United kufanya makubwa katika mechi hiyo kwa sababu kiuhalisia United ni klabu kubwa ambayo ina mifumo yenye kuweza kuivuruga kabisa Barcelona kwenye michuano hiyo.


Rehema
Asante meridianbet kwa taarifa
Nasra
Asantee