Hazard Huyooo…!

Inaonekana kabisa kwamba baada ya Zidane kuwasili Blancos hapo kuna mazungumzo ya mwanzo yamejadiliwa ili kuangalia kama mchezaji huyo ataweza kutua Bernabeu huku kocha huyo akiwa amekabidhiwa kikosi hicho akifanyie urejeshaji ili kurudisha nidhamu na mafanikio ya klabu hiyo kwa ujumla.

Hazard, ikumbukwe, ni miongoni mwa wachezaji wachache wanaowindwa na klabu hiyo ikiwa kwao ni kama mbadala wa kukipa nguvu kikosi hicho kilichokosea hatua za awali kwa kumwondoa Ronaldo baada ya mchezaji huyo kutimkia Italia na kuona ni bora kuwa na radha tofauti.

Waliwezaje?

Wameweza kuishi kikosini hapo bila kocha huyo kwa miezi kumi na klabu yao ikishindwa kabisa kufanya vizuri ndipo wakachukua maamuzi ya kutafuta namna ya kumshawishi ili arudi kikosini hapo kuokoa jahazi hilo na wakatumia ushawishi wa kumfanya mchezaji huyo aweze kutua katika jiji lao la Madrid.

Ni ukweli usiopingika kwamba kocha huyo hawezi kuendelea kukubali kukaa na kikosi ambacho hakina nyota mwenye uwezo wa kuifanya timu ipate matokeo. Ni vigumu kwa mwalimu yeyote kukubaliana na hali hiyo; ndiyo maana imekuwa rahisi kwake kupata kikosi anachoona yeye kinaweza kuleta makombe.

Hazard Huyooo…!

Sio eneo la ushambuliaji pekee ambalo Madrid wamekuwa wakiliangalia lakini wanaona kuna walakini pia katika maeneo mengine ambayo wanaonelea kuna haja ya kuongeza nguvu kama vile eneo la ulinzi ambapo wamejaribu kuandaa wachezaji wawili ambao ni Matthis de Ligt na Kalidou Koulibaly japo kuna ushindani kidoho kutoka klabu nyingine kama United.

Eneo gani lingine la maboresho?

Pia, wameona kuna haja ya kuongeza nguvu eneo la kiungo ambalo kwa namna ya pekee limekuwa likifanya vizuri kutokana na kuwa na wachezaji kama vile Kroos, Modric na Casemiro ambao bado wanafanya vizuri lakini wanahitaji changamoto ya mchezaji mpya ili kuongeza ubunifu zaidi ndani ya kikosi hicho. Na wameonelea Eriksen anaweza kuwa sahihi kwa nafasi hiyo.

Wengine ambao klabu hiyo ilitamani kuwa nao ni Neymar na Mbappe lakini itakuwa ngumu sana kuwapata kutokana na madai makubwa kusonga kwenye biashara hiyo kuu. Hivyo, katika hali ya kawaida wanatakiwa kuangalia wachezaji ambao tayari wamejenga uzoefu mkubwa kwenye michuano mingine ya kusaka nafasi za kujizatiti kiubora. Watakachokifaidi kwa Hazard ni kwamba mkataba wake wa sasa unaisha 2020 hivyo gharama zake haziwezi kuwaumiza Madrid.

Anatabiriwa makubwa sana ndani ya klabu hiyo endapo atafanikiwa kutua hapo chini ya Zidane maana sio mchezaji wa kiwango cha kushuka bali ni mchezaji ambaye anakua kadri siku zinavyosonga. Ni chaguo zuri kwa Madrid katika kipindi hiki.

4 Komentara

    Harzad anajua.

    Jibu

    Harzad yuko vizuri sana akiwa uwanjan anajua nin cha kufanya anajituma sana

    Jibu

    Eden hazard yuko vzr sana ila kwa kwenda real Madrid sio jambo jema bora angebaki the blues kwa Madrid watu sahihi kama wanataka kurudisha makali yao bora wawasajili hawa wawili klyn mbappe na jr neymar itakua bora zaid

    Jibu

    Noma sana hiiiii

    Jibu

Acha ujumbe