Messi amekuwa na bahati mbaya akirejea kikosini Argentina kwa kushindwa kuona nyavu huku akipata jeraha wakati timu yake ya taifa ikikubali kichapo cha bao 3-1 dhidi ya Venezuela.
Nyota huyu wa Barcelona alikosa kushiriki mechi sita za timu yake ya Taifa baada ya kuchapwa na mabingwa Ufaransa kwenye fainali za kombe la Dunia 2018.
Messi amekuwa hana bahati wakati huu ambao aliamua kurejea kuitumikia timu yake ya taifa ya Argentina kwenye gemu ilizokuwa nazo mbele yake. Licha ya kmuwa staa huyu aliweza kumaliza gemu lakini alishindwa kupata goli kama matarajio ya wengi yalivyokuwa.
Messi pia anatarajia kuikosa gemu ya kirafiki dhidi ya Morocco kwa sababu ya jeraha alilo nalo japokuwa linalipotiwa kuwa jeraha hilo sio shida kubwa sana.
Zeiyana
Niwakati mgumu sana kwake messi..!pole sana utapona utarudi kwenye ali yako ya kawaida