Kocha mkuu wa Ureno Fernando Santos hajafurahishwa na matokeo ambayo timu yake wameyapata dhidi ya Ukraine Ijumaa. Katika kuzungumzia sababu za kukosa ushindi anasema yeye anaitazama timu nzima kwa ujumla wake, akikataa kuonesha kuwa alimzingatia Ronaldo pekee.
Kwenye ufunguzi wa kufuzu Euro 2020 Ronaldo alirejea Ureno kuwasaidia kutoboa kwenye gemu yao dhidi ya Ukraine, lakini hawakubahatika kupata goli au ushindi. Ureno walitoa sare ya 0-0 dhidi ya Ukraine ijumaa, Santos amepuuza baadhi ya msisitizo unaowekwa na wadau kuhusu uchezaji wa Ronaldo kwenye gemu hiyo.
Kuhusu Ronaldo, De santos anasema hakuna haja ya kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja, kwa upande wake anaona kama wachezaji walikuwa hawajaridhika, na Ronaldo ni sehemu ya timu.
Santos anasema licha ya kuwa wachezaji wana uzoefu mkubwa katika klabu zao kubwa lakini hawakuridhika na ndio maana wakashindwa kufanya vizuri. Yeye anasema anatazama namna ambavyo wanaweza kushinda mechi zingine ambazo zipo mbele yao na wanaweza kufanya hivyo wakiwa na Ronaldo au wasipokuwa naye.


Povel
Cr7 mnyama sana