Jose Mourinho: Najiandaa kwa Kibarua Kipya

Aliyekuwa meneja wa Manchester United kabla hajatimuliwa Jose Mourinho, sasa anasema yupo katika maandalizi ya kukipokea kibarua kingine cha umeneja katika msimu wa joto unaokuja.

Bwana huyu ambaye pia amewahi kuwa meneja wa klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan ameshadaiwa kuzikataa ofa kadhaa zilizomfuata mapema kabisa baada ya kutimuliwa klabuni hapo.

Jose anasema yeye anaelewa nini anataka na nini hgataki, hivyo anajiandaa kuingia kibaruani msimu wa joto na anasubiri ofa nono zaidi ili aweze kwenda nayo sambamba. Mourinho baada ya kutimuliwa na United ameendelea kufurahia kujihusisha na soka kama mchambuzi katika vituo mbalimbali alivyokuwa akialikwa.

“Nitapendelea zaidi kurejea mwezi Juni, msimu wa joto mwanzoni kabisa mwa msimu. Ninafanya kazi, ninajiandaa kwa kazi nyingine msimu ujao”

Mourinho alikuwa akihusishwa na kurejea kule Real Madrid kabla klabu hiyo haijaamua kumrejesha Zinedine Zidane. Hata hivyo, ukiacha vibarua vinne anavyodaiwa kukataa, Jose anaripotiwa kuwa alikataa dili la kufundisha timu ya taifa pia.

2 Komentara

    Namkubali sana hyu kocha morinho

    Jibu

    Habar njema kwake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.