Mnyama Atafunwa!

 

Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mazuri ndani ya ligi na baadhi ya mechi za kimataifa klabu ya Simba imekubali kupokea kichapo kingine mbele ya Waalgeria, J. S. Soura katika michuano ya klabu bingwa Afrika inayoendelea kuunguruma katika viwanja tofauti tofauti vya vilabu vinavyoshiriki michuano hiyo mikubwa sana Afrika.

Gemu ilikuwaje?

Katika mchezo huo Simba walionekana kutawaliwa katika kila idara kutokana na klabu ya Soura kuwa makini sana wakati wote wa mchezo kuhakikisha kwamba hawawaangushi kabisa mashabiki wao waliokuwa na hamasa kubwa ya mchezo, kuipa nguvu timu yao ambayo katika mechi ya mwanzo walipoteza mchezo huo.

Walikuwa ni Soura ambao walionesha uwezo wa hali ya juu katika mechi hiyo mara baada ya kumiliki sana mpira na kuwapa kashikashi wachezaji wa klabu ya Simba ambao walionekana kupoteza kabisa uelekeo wa mechi hiyo kutokana na kuwaruhusu wenyeji hao kuwashambulia kwani mara kwa mara walilisakama lango la mpinzani wao.

Alikuwa ni Yahia Cherif ambaye dakika ya 18 tu alitikisa nyavu za Wekundu hao wa Msimbazi wakati wa mechi baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa kikosi hicho cha Simba baada ya kumpa mpira uliomfanya kupiga shuti lililomfanya mlinda mlango kukosa la kufanya na kuwaacha wenyeji kuwa mbele yao.

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Soura walikuwa mbele kwa goli moja ambalo liliwafanya wenyeji hao kuondoka na ushindi kwa kipindi cha kwanza baada ya kuonekana wamefanikiwa kutumia mbinu za mwalimu wao za kushambulia kwa kasi ya ajabu na kucheza mpira mwingi ambao ungeweza kuwachosha wachezaji wa timu pinzani.

Kipindi cha pili kilirudi kwa kasi ya ajabu ambapo kila timu ilijitahidi kutafuta goli ambalo lingewaweka katika nafasi nzuri ya kukaa juu ya jedwali la ubingwa huo wa Afrika. Japo mambo yalionekana magumu kwa Simba ambaye aliweza aliweza kuwapa mazingira ya kupata penati wapinzani wake katika dakika ya sita tu ya kipindi cha pili.

Wakati wote uliobaki timu zilikuwa zikishambuliana kwa zamu huku Soura wakijaribu kutafuta magoli zaidi ndani ya mchuano huo huku Wekundu wa Msimbazi wakifanya kila linalowezekana kurudi kwenye mstari angalau wapate goli la kufutia machozi kitu ambacho kilionekana kigumu kwao kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya wenyeji hao.

Msimamo

Kwa ushindi huo ambao J. S. Soura wameupata wamewashusha Simba hadi nafasi ya mwisho kwenye kundi lao kutokana na kuzidiana alama, pia katika kundi lao, Al Ahly walikubali kibano cha 1-0 kutoka kwa wenyeji AS Vita ambao waliwafunga katika dakika za lala salama za mchezo huo uliokuwa mgumu sana baina ya pande hizo mbili. Kwa sasa kundi limebaki kuwa gumu huku kila mmoja akitegemea matokeo ya mechi yao ya mwisho ili kujua nafasi yake ya kusonga mbele.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.