Zinedine Zidane ameendelea kuzipa moto taarifa za yeye kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Juventus ambayo anatajwa kuwa namba moja kwenye nani atarithi kliti cha meneja wa klabu hiyo, inadaiwa ameshatua Italia.
Zidane aliyekuwa meneja wa Zamani wa Real Madrid, ambaye kwa mda fulani hivi sasa amekuwa hana klabu amekuwa akihusishwa naklabu mbalimbali, ikiwepo Juventus, Man Udt na Chelsea.
Kibarua cha Max Allegri kinatajwa kuwa mashakani kufuatia matokeo mabaya ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid Jumanne iliyopita.
Kwa mujibu wa jarida la La Stampa, Zidane amekuwepo Turin kwa siku kadhaa sasa. Taarifa zinadai pia licha ya majukumu yake mengine alipata nafasi ya kuonana na wawakilishi wa klabu ya Juventus na kufanya mazungumzo.
Taarifa zinaripoti kuwa Zinedine Zidane hajapata wasaa wa kuonana na raisi wa Juventus Andrea Agnelli na kufanya naye mazungumzo moja kwa moja, lakini kama amefanya mazungumzo na wawakilishi wake huenda wakawa wamezungumza kwa upana zaidi.
Kuna taarifa kuwa Real Madrid wanamuhitaji Zidane arejee klabuni hapo kuchukua nafasi ya Santiago Solari ambaye hana bahati sana toka alipoingia klabuni hapo. PSG pia wanatajwa kuwa kwenye mbio za kumwania Zidane kuwa meneja wao.


Zeiyana
Zidane ni kocha ambaye kila mchezaji hanavutiwa sana akiwa kwenye clabu yake