Ajax Kumchukua Sergio Roberto

Klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi ipo kwenye mazungumzo na mchezaji wa klabu ya Barcelona Sergio Roberto raia wa kimataifa wa Hispania wakimshawishi kujiunga nao.

Sergio Roberto inaelezwa atatimka ndani ya klabu ya Barca na Ajax ni moja ya vilabu ambavyo vinafukuzia huduma ya mchezaji huyo kueleka msimu wa 2024/25, Hivo kama mazungumzo yao yatakwenda vizuri basi bila shaka mchezaji huyo atajiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Uholanzi.ajaxMchezaji huyo ambaye ameibuliwa kutoka akademi ya Barcelona ameitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu sasa tangu mwaka 2010 ikiwa ndio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kucheza timu ya wakubwa ya Barcelona, Hivo klabu hiyo na mchezaji mwenyewe wanaelezwa kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana.

Inaelezwa mchezaji Sergio Roberto ataangalia vilabu vyote ambavyo vimekua vikimuhitaji na yeye kuchagua ni klabu gani ambayo ataichagua kuitumikia baada ya kudumu ndani ya Barcelona kwa miaka takribani 14, Lakini mpaka sasa klabu ya Ajax ndio wanaongoza kinyang’anyiro cha kumuwania mchezaji huyo.

Acha ujumbe