Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema mapumziko ya mechi za kimataifa yanasababisha majeraha sana kwa wachezaji kwakua wanakosa mda wa kupumzika na wanachoka sana.
Carlo Ancelotti yeye anaamini mechi za kimataifa zinapeleka wachezaji wengi kuchoka sana na kukosa kwao muda wa mapumziko kunapelekea wao wachezaji kupata majeraha sana.Kocha huyo ameyazungumza hayo wakati akizungumzia jeraha la beki wake David Alaba ambaye alipata jeraha katikati ya wiki dhidi ya klabu ya Las Palmas na kusema kua jeraha sio kubwa sana na anaweza kurejea katika mchezo dhidi ya Napoli.
Klabu ya Real Madrid karibuni imekua ikikumbana na tatizo la wachezaji wake kupata majeraha sana kwani wachezaji wake muhimu kama Thibaut Courtois, David Alaba, Eder Militao, pamoja na Vinicius Jr ambaye amerejea uwanjani hivi karibuni.Kocha Carlo Ancelotti ambaye anaiongoza klabu ya Real Madrid kwa msimu wa tatu sasa, Yeye anaamini kua wachezaji wanapata majeraha sana kutokana na michezo ya kimataifa ambayo inaambatana na michezo ya ligi bila wachezaji kupumzika.