Ancelotti: Hatuna Mpango wa Kusajili

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameweka wazi hawana mpango wa kusajili mchezaji yeyote kwenye kikosi hicho kuelekea siku za mwisho za dirisha kufungwa.

Ilifikiriwa kua klabu ya Real Madrid inawezas kuongeza mchezaji kuelekea mwisho wa dirisha la usajili haswa kwenye eneo la ulinzi, Lakini kocha Ancelotti ameweka wazi hawana mpango wa kuongeza mchezaji kwenye eneo hilo kwakua wana wachezaji wazuri akiwataja wachezaji kama Tchouameni, Jacobo, na Ascensio.ancelottiKlabu ya Real Madrid ilikua inahusishwa na wachezaji kadhaa wa eneo la ulinzi kwenye dirisha hili ikiwemo Leny Yoro ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United, Inasemekana mchezaji huyo ndio alikua pekee kwenye mipango ya Madrid hivo kumkosa kumefanya mabingwa hao wa ulaya kuachana na mpango wa kusajili beki.

Real Madrid wameanza kuandamwa na majeraha kwenye kikosi chao na pengine ikawa ndio sababu ya waandishi wa habari kumuuliza Ancelotti juu ya kuongeza mchezaji mpya ndani ya timu hiyo, Lakini kocha huyo amesisitiza hawana mpango wowte wa kusajili mchezaji kuelekea dirisha la usajili kufungwa.

Acha ujumbe